Ruka kwenda kwenye maudhui

Safio inavyofanya kazi

Jinsi ya kuanza kutumia Safio kwenye dobi lako

Jisajili mtandaoni, weka huduma zako na utume uthibitisho wa biashara yako. Safio ikishauidhinisha, unaweza kupokea oda na kurekodi malipo. Hizi ndizo hatua zote, na unachopaswa kuandaa.

Hatua tano kuanzia usajili hadi oda yako ya kwanza

  1. Sajili dobi lako

    Jina lako, jina la dobi lako, namba ya simu na barua pepe. Mpango wa Starter ni bure na hauhitaji kadi.

  2. Kamilisha uthibitisho wa biashara

    Pakia nyaraka za biashara yako. Mtu wa Safio anazikagua; zikiidhinishwa unaweza kupokea oda na malipo. Una swali ukisubiri? Tuandikie WhatsApp.

  3. Weka huduma na bei

    Mashati, suti, mashuka, kufua na kukunja kwa kilo: kwa bei unazotoza tayari.

  4. Anza kupokea oda za kaunta

    Kaunta, kwa simu au WhatsApp. Rekodi kilicholipwa na uchapishe risiti.

  5. Fuatilia hesabu za biashara yako

    Tumia ripoti ya siku, na kwenye mipango ya kulipia ripoti za wiki na mwezi, kuona biashara inavyokwenda.

Uthibitisho wa biashara

Uthibitisho unamaanisha nini

Mtu wa Safio anakagua taarifa na nyaraka za biashara yako. Ukaguzi huu unafanywa na mtu, kwa hiyo akaunti yako inaweza kupokea oda na malipo baada ya kuidhinishwa tu, si mara tu unapojisajili.

Unachopaswa kuandaa

Unachagua biashara yako ilivyosajiliwa na unaombwa tu kile kinachoihusu:

Kampuni yenye ukomo (Ltd)
Cheti cha usajili cha BRELA, cheti cha TIN, leseni ya biashara na kitambulisho cha mtu anayewajibika, pamoja na namba ya usajili na TIN.
Jina la biashara lililosajiliwa
Usajili wa BRELA, leseni ya biashara na kitambulisho cha mtu anayewajibika, pamoja na namba ya usajili na TIN.
Mfanyabiashara binafsi
Kitambulisho cha mmiliki na uthibitisho wa anwani ya eneo la biashara.

Kila mtu pia anatoa jina lililosajiliwa, anwani na mkoa, na jina na wadhifa wa mtu anayewajibika. Fomu ya uthibitisho ndani ya Safio Business inaorodhesha hasa kinachokuhusu. Nyaraka zinahifadhiwa kwa usimbaji fiche kwenye hifadhi ya faragha.

Nini kinatokea baada ya kuwasilisha

  • Unaweza kuandaa wasifu, huduma, bei na wafanyakazi wako ukisubiri. Oda na malipo yanafunguliwa baada ya kuidhinishwa.
  • Timu ya Safio inakagua uthibitisho ndani ya siku chache za kazi. Utaona matokeo kwenye ukurasa wa Uthibitisho ndani ya Safio Business.
  • Kama kuna cha kurekebisha, mkaguzi anakuambia ni nini, nawe unasahihisha na kuwasilisha tena.
  • Ukishaidhinishwa, unaweza kupokea oda na kurekodi malipo.

Unahitaji msaada wa kujisajili?

Tuandikie WhatsApp au piga simu +255 768 505 988, kwa Kiswahili au Kiingereza.

Loading Safio · Inapakia Safio